Yosefu Barsaba
Yosefu Barsaba (pia Yusto, yaani "Mwadilifu") alikuwa mmojawapo kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu.
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a4/70Apostles.jpg/220px-70Apostles.jpg)
Kwa msingi huo, baada ya kifo cha Yuda Iskarioti, akawa mmoja kati ya wawili waliopendekezwa kushika nafasi yake kama mtume, lakini bahati ilimuangukia Mathia (Mdo 1:21-26).
Hata hivyo alifanya bidii katika uinjilishaji[1]. Mapokeo ya Kikristo yanasimulia kwamba baadaye akawa askofu wa Eleutheropoli, alipofia dini.
Anaheshimiwa hivyo na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waarmenia kama mfiadini kwa jina la mtakatifu Yusto wa Eleutheropoli. Aliweza kuwa mmojawapo kati ya wakazi wengi waliouawa na Vespasian mwaka 68[2].
Sikukuu yake huadhimishwa nao tarehe 20 Julai[3], 30 Oktoba na 9 Aprili.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
![]() | Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yosefu Barsaba kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoAina za manenoKumaShairiKamusi za KiswahiliDiamond PlatnumzMaumivu ya kiunoInsha ya wasifuSimba S.C.Fasihi simuliziIdd el HajjTanzaniaOrodha ya Watakatifu WakristoHifadhi ya mazingiraMikoa ya TanzaniaMaalum:MabadalikoyaKaribuniKisaweNembo ya TanzaniaMapenziJohn Raphael BoccoMapenzi ya jinsia mojaTendo la ndoaVivumishiUandishi wa ripotiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMazingiraMpira wa miguuMshororoVitendawiliOrodha ya makabila ya TanzaniaMadawa ya kulevyaMasoud KipanyaKiswahiliNahauMofimuVita Kuu ya Pili ya Dunia