Yeriko

Yeriko (kwa Kiebrania יְרִיחוֹ, kwa Kiarabu أريحا, maana yake "wenye kunukia") ni mji wa kale sana, ulioanzishwa miaka 9000 hivi KK karibu na mto Yordani.

Yeriko kutoka kusini.

Mwaka 2006 ulikuwa na wakazi 20,400[1][2]

Upekee wake

Umaarufu wake unatokana na kuwa chini ya usawa wa bahari kuliko miji yote duniani.

Unasadikiwa pia kuwa mmojawapo kati ya miji ya zamani zaidi kukaliwa mfululizo hadi leo.[3][4][5]

Akiolojia imekuta chini ya ardhi zaidi ya miji 20 iliyojengwa kwa nyakati tofauti mahali pale, kuanzia miaka 11,000 iliyopita.[6]

Katika Biblia

Katika Biblia unatajwa kama "Mji wa Mitende": chemchemi mbalimbali ndani na kandokando yake zilivuta binadamu tangu milenia nyingi.[7]

Katika Agano la Kale unatajwa kwa namna ya pekee kuhusiana na Yoshua kuingiza Waisraeli waliotoka Misri katika nchi ya Kanaani kwa kuvuka mto Yordani mkabala wa Yeriko na kuuteka kwa maandamano ya ibada (Yos 6) kabla ya miji mingine yoyote.

Katika Agano Jipya unatajwa kuhusiana na Yesu ambaye huko alimuongoa mtozaushuru tajiri Zakayo (Luk 19) na kumponya kipofu ombaomba Bartimayo (Mk 10).

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: