Walowezi

Walowezi (kutoka kitenzi "kulowea"; pia: setla, kutoka Kiingereza "settler") ni watu ambao wamehamia katika eneo fulani na kuanzisha makazi ya kudumu pale, hata mara nyingi kulitwaa eneo hilo. Makazi mara nyingi hujengwa kwenye ardhi ambayo inadaiwa au inayomilikiwa na watu wengine.

Picha inayoonyesha walowezi wa kwanza wa Karne za kati wakifika Aisilandi.

Wao wenyewe wakati mwingine huondoka katika kujitafutia riziki au uhuru wa dini[1].

Mara nyingine walowezi huungwa mkono na serikali au nchi kubwa au tajiri[2].

Sababu za uhamiaji

Sababu za kuhama kwa walowezi hutofautiana, lakini mara nyingi huwa ni mambo yafuatayo: hamu ya mwanzo mpya na maisha bora katika nchi ya kigeni, hali duni ya kifedha, dhuluma ya kidini[1], ya kijamii, ya kiutamaduni au ya kikabila[2], kukandamizwa kisiasa, na sera kutoka serikali zinazowapa motisha wananchi kwa lengo la kuhamasisha makazi ya kigeni.[3]

Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Walowezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.