UN Women

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wanawake na wasichana

UN Women ni shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika kuwawezesha na kutetea haki na usawa kwa wanawake na wasichana, pamoja na upingaji wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Shirika hili la kimataifa la uwewezeshaji Wanawake Duniani lilianzishwa mnamo mwaka 1976 na kutambuliwa rasmi mwaka 1976 na kuanza kufanya kazi zake rasmi mnamo mwezi Januari mwaka 2011 .[1]Raisi mstaafu wa Chile Michelle Bachelet alikuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika hili, na Sima Sami Bahous ni mkurugenzi mtendaji wa shirika hili kwa sasa.[2] Shirika hili pia ni mwanachama wa kundi la kimaendeleo la umoja wa Mataifa .[3]

Marejeo