Thebai lilikuwa jina la Kigiriki, Wamisri wa Kale waliita Waset , ambayo ilikuwa pia jina la mkoa katika Misri ya juu.
Wakati wa Ufalme wa Kati, Farao Mentuhotep II alifanya Waset - Thebes kuwa mji mkuu wa Misri.
Hapo mahekalu makubwa yalijengwa au kupanuliwa ambayo yanaonekana hadi leo. Hasa mahekalu ya Karnak na Luxor hutembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka dunia yote.
Thebes - Waset ilirudi kuwa mji mkuu mara kadhaa baada ya Mehutep II. Kuna uwezekano kwamba mnamo mwaka 1500 KK Thebes ilikuwa mji mkubwa zaidi duniani kwa wakati wake, ikiwa na wakazi 75,000[1]. Iliharibika wakati wa uasi dhidi ya mfalme Ptolemaio IX mnamo mwaka 84 KK; wakati wa Dola la Roma kikosi cha jeshi kilikaa katika hekalu la kale la Karnak. Mji wa Luxor ya leo ilikuwa kijiji kilichobaki kando ya hekalu la Luxor.
Gauthier, Henri. 1925-1931. Dictionnaire des noms géographiques contenus dans les textes hiéroglyphiques . Juzuu. 3 ya 7 vols. Cairo: Imprimerie de l'Institut français d'archéologie orientale du Caire. (Ilichapishwa tena Osnabrück: Otto Zeller Verlag, 1975). 75, 76.
Polz, Daniel C. 2001. "Thebes". Katika The Oxford Encyclopedia ya Misri ya kale, iliyohaririwa na Donald Bruce Redford. Juzuu. 3 ya 3 vols. Oxford, New York, na Cairo: Chuo Kikuu cha Oxford Press na Chuo Kikuu cha Amerika huko Cairo Press. 384-388.
Redford, Donald Bruce. 1992. "Thebes". In The Anchor Bible Dictionary, iliyohaririwa na David Noel Freedman. Juzuu. 6 ya 6 vols. New York: Doubleday. 442–443. (seti ya ujazo 6)
Strudwick, Nigel C., & Strudwick, Helen, Thebes huko Misri: Mwongozo wa Makaburi na Mahekalu ya Luxor ya Kale . London: Jumba la Habari la Jumba la kumbukumbu la Briteni, 1999, ) / (karatasi)
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Thebes kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.