The Proposal

The Proposal ni filamu ya kuchekesha iliyotolewa 2009, iliyoongozwa na Anne Fletcher na kuigizwa na Sandra Bullock na Ryan Reynolds. Filamu hii ilitungwa na Pete Chiarelli.[2]

The Proposal
Imeongozwa naAnne Fletcher
Imetayarishwa naTodd Lieberman
David Hoberman
Alex Kurtzman
Roberto Orci
Kristin Burr
Imetungwa naPeter Chiarelli
NyotaSandra Bullock,
Ryan Reynolds,
Malin Akerman
Mary Steenburgen
Craig T. Nelson
Betty White
Oscar Nuñez
Aasif Mandvi
Muziki naAaron Zigman
Imehaririwa naAmanda Mackey Johnson
Cathy Sandrich
Imesambazwa naTouchstone Pictures
Imetolewa tar.Juni 1, 2009 (2009-06-01)
Ina muda wa dk.Dakika 108
NchiMarekani
LughaKiingereza
Bajeti ya filamu$40 million[1]
Mapato yote ya filamu$314,658,031[1]

Hadithi

Margaret Tate ni mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu inayoitwa Ruick & Hunt Publishing. Wafanyikazi wake hawapendi uongozi wake. Baada ya kupata habari kuwa atarudishwa kwao nchini Canada, yeye anamlazimisha mtumishi wake, Andrew Paxton, amuowe ili apate kubaki nchini Marekani. Andrew anakubali kumuoa Margaret, lakini kwa masharti.

Wawili hawa wanaenda likizo kwa wazazi wa Andrew, kijijini Sitka, Alaska ili kuwadangaya familia yao kuwa wanaowana. Margaret anashikwa na bumbuwazi pindi anapogundua kuwa familia ya kina Andrew ni matajiri wanaomiliki biashara nyingi kijijini Sitka. Baada ya sherehe iliyoandaliwa nyumbani, Andrew anatangaza kuwa atamuowa Margaret.

Familia ya Andrew ilipokea habari hizo kwa furaha (isipokuwa babake Andrew) na wanapanga kuwa harusi ifanywe wiki hiyo hiyo.Harusi inapofanyika Margaret anaamua kuwa hawezi kuolewa na Andrew, na anatubia mbele ya kila mtu kuwa hiyo ilikuwa harusi ya uwongo. Margaret anaarifiwa kuwa ana saa 24 za kurudi Canada. Kwa sababu Margaret alikubali hatia aliyofanya, Andrew hakupelekwa jela. Margaret alirudi New York, na kufunganya vitu vyake. Andrew anakimbilia kumfuata na anampata Margaret ofisini anapomuambia kuwa anampenda mbele ya watu wote ofisini. Andrew anamposa Margaret, na wawili hawa na wachumba, na mara hii ni "kikwelikweli".

Waigizaji

  • Sandra Bullock aliigiza kama Margaret Tate, mhariri mkuu wa kampuni ya kuchapisha vitabu.
  • Ryan Reynolds aliigiza kama Andrew Paxton, anayekubali kumuoa Margaret kwa sharti la kupandishwa cheo cha mhariri.
  • Mary Steenburgen anayeigiza kama Grace Paxton, mamake Andrew.
  • Craig T. Nelson aliigiza kama Joe Paxton, babake Andrew anayemtaka Andrew amiliki biashara alizonazo kijijini Sitka.
  • Betty White aliigiza kama Annie, nyanyake Andrew.

Kurekodi filamu

Ingawa filamu hii ilichukuliwa kijijini Sitka, filamu hii ilirekodiwa katika eneo la Cape Ann mjini Massachusetts.

Muziki

Ilitungwa na Aaron Zigman aliyerekodi nyimbo zake kwenye studio ya Hollywood Studio Symphony.[3]

Mafanikio

Kwenye siku yake ya kwanza, filamu hii iliuza tikiti za milioni $12.7 kutoka kwa sinema 3,056, na kuwa namba 1 siku hiyo..[1][4] Filamu hii ilipata milioni $314 kote duniani na kuifanya filamu mojawapo ya Sandra Bullock iliyopata mafanikio iliyokusanya $163,958,031 kutoka nchi ya Marekani na Canada.

DVD

The Proposal ilitolewa kwa DVD mnamo 13 Oktoba 2009.[5] Baada ya wiki mbili, iliuza nakala za DVD 3,314,840 na kupata $54,744,965.[6]

Tuzo

Sandra Bullock alichaguliwa kwa tuzo la Golden Globe Award na akashinda tuzo la Teen Choice Award..[7] Pia, alishinda tuzo la People's Choice Award kwa kuwa muigizaji bora.

Marejeo

Viungo vya nje