Shirika la Mkombozi

Shirika la Mkombozi Mtakatifu sana (kwa [[Kilatini: Congregatio Sanctissimi Redemptoris – Ufupisho: C.Ss.R au CSSR) ni shirika la kitawa la kimisionari la Kanisa Katoliki lililoanzishwa na Alfonso Maria wa Liguori tarehe 9 Novemba 1732 huko Scala (karibu na Amalfi, Italia) ili kushughulikia watu waliosahaulika wa mkoa wa Napoli.

Mt. Alfonso Maria wa Liguori (1696-1787), Mwanzilishi wa shirika
Mt. John Nepomucene Neumann (1811-1860), askofu wa kwanza wa Marekani kutangazwa mtakatifu

Kwa Kiingereza wanashirika wanajulikana kama Redemptorists. Wakiwa mapadri na mabradha wanafanya kazi katika nchi zaidi ya 77 duniani kote. Mkuu wao anaitwa Michael Brehl.

Wanashirika maarufu

  • Mtakatifu Alfonso Maria wa Liguori (1696-1787) Mwanzilishi, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
  • Mtakatifu Jeradi Majella (1726-1755) bradha
  • Mtakatifu Klement Hofbauer (1751-1888) padri
  • Mtakatifu John Nepomucene Neumann (1811-1860) Askofu
  • Mwenye heri Peter Donders (1809-1887) padri
  • Mwenye heri Kaspar Stanggassinger (1871-1899) padri
  • Mwenye heri Gennaro Maria Sarnelli (1702-1744) padri
  • Mwenye heri Nicholas Charnetsky (1884-1959) Askofu na mfiadini
  • Mwenye heri Vasyl Velychkovsky (1903-1973) Askofu na mfiadini
  • Mwenye heri Zenon Kovalk (1903-1941) padri na mfiadini
  • Mwenye heri Ivan Ziatyk (1899-1952) padri na mfiadini
  • Mwenye heri Francis Xavier Seelos (1819-1867) padri

Viungo vya nje