Sebi

Sebi (625 hivi - 695) alikuwa mfalme wa Essex (leo nchini Uingereza) tangu mwaka 664 hadi 694.

Alishika imani na ibada ya Kikristo bila kujali lawama za Wapagani, na hatimaye, alipokubaliwa na mke wake, aling'atuka ili kujiunga na monasteri hadi kifo chake kama alivyotamani kwa muda mrefu [1].

Anaheshimiwa na baadhi ya madhehebu ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe 29 Agosti[2].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.