Salamu Maria
Salamu Maria (kwa Kilatini Ave Maria) kwa asili ni sala ya Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini ambayo inamsifu Bikira Maria na kumuomba sala zake hadi saa ya kufa.
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/96/Fra_Angelico_069.jpg/200px-Fra_Angelico_069.jpg)
Sala hiyo imeenea hata kwa Wakristo wengine, hasa Waanglikana, lakini kwa namna tofauti inatumiwa pia katika Ukristo wa Mashariki.
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya sala hiyo inatokana na Injili (Lk 1:28,42) moja kwa moja:
- Χαῖρε, κεχαριτωμένη, ὁ Κύριος μετὰ σοῦ / Chaire, kecharitōmenē, o Kyrios meta sou / Salamu uliyejaa neema, Bwana yu nawe (maneno ya Malaika Gabrieli)
- Εὐλογημένη σὺ ἐν γυναιξὶν καὶ εὐλογημένος ὁ καρπὸς τῆς κοιλίας σου / eulogēmenē su en gynaixin kai eulogēmenos o karpos tēs koilias sou / Umebarikiwa wewe kati ya wanawake na umebarikiwa mzao wa tumbo lako (maneno ya Elizabeti)
Katikati ya karne ya 13 sala ilikuwa inaundwa na maneno hayo tu pamoja na kuingiza jina la Maria, inavyoonekana katika ufafanuzi wa Thoma wa Akwino.[1]
Mwishoni mwa karne ya 15 yaliongezwa maneno ya kumuomba Maria sala zake.[2]
Hatimaye sala kwa Kilatini imekuwa hivi:
- Áve María, grátia pléna,
- Dóminus técum.
- Benedícta tu in muliéribus,
- et benedíctus frúctus véntris túi, Iésus.[3]
- Sáncta María, Máter Déi,
- óra pro nóbis peccatóribus,
- nunc et in hóra mórtis nóstrae. Ámen.
Tafsiri ya Kiswahili ni:
- Salamu María, umejaa neema,
- Bwana yu nawe.
- Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
- na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
- Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu,
- utuombee sisi wakosefu,
- sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Tanbihi
Viungo vya nje
- University of Dayton Hail Mary in various languages Archived 16 Februari 2013 at the Wayback Machine.
![]() | Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Salamu Maria kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoAina za manenoKumaShairiKamusi za KiswahiliDiamond PlatnumzMaumivu ya kiunoInsha ya wasifuSimba S.C.Fasihi simuliziIdd el HajjTanzaniaOrodha ya Watakatifu WakristoHifadhi ya mazingiraMikoa ya TanzaniaMaalum:MabadalikoyaKaribuniKisaweNembo ya TanzaniaMapenziJohn Raphael BoccoMapenzi ya jinsia mojaTendo la ndoaVivumishiUandishi wa ripotiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMazingiraMpira wa miguuMshororoVitendawiliOrodha ya makabila ya TanzaniaMadawa ya kulevyaMasoud KipanyaKiswahiliNahauMofimuVita Kuu ya Pili ya Dunia