Roskosmos

Roskosmos (rus. Роскосмос) ni jina la kifupi la shirika la serikali ya Urusi kwa shughuli za kiraia kwenye anga-nje. Jina kamili kwa Kirusi ni Государственная корпорация по космической деятельности (gosudarstvenaya korporatsiya po kosmocheskoi deyatelnosti "shirika ya kiserikali ya shughuli za angani").

Nembo ya Roskosmos

Shirika hili lilianzishwa tarehe 1 Januari 2016 kwa amri ya rais Putin likachukua nafasi ya mamlaka ya kitangulizi yenye jina lilelile.[1][2]ROSKOSMOS iliyounganishwa na Shirika la Roketi na anga-nje (Объединенная ракетно-космическая корпорация, United Rocket and Space Corporation)iliyowahi kutengeneza vyombo vya anga.

Roskosmos mpya inahusika na miradi yote ya kiraia (tofauti na miradi ya kijeshi) ya Urusi kwenye anga. Makao makuu yapo Moscow na kituo cha kufunza wanaanga kipo kwenye "Mji wa nyota" (Swjosdny Gorodok). Kituo cha kurusha roketi kinapatikana Baikonur nchini Kazakhstan iliyokuwa kituo cha Umoja wa Kisovyeti.

Kwa ujumla shirika la Roskosmos linachukua nafasi ya taasisi mbalimbali zilizohusika zamani ya ukomunisti katika Umoja wa Kisovyeti kupanga, kutengeneza na kutoa roketi na vyombo vya angani kama vile Sputnik 1, Soyuz na MIR.

Wanaanga Warusi (zamani za Umoja wa Kisovyeti)

Marejeo

Viungo vya Nje