Rhythm Divine

"Rhythm Divine" ni single ya kwanza iliyotolewa na Enrique Iglesias kutoka katika albamu yake ya lugha ya Kiingereza, Enrique. Kibao hiki kilitungwa na kutayarishwa na kikosi kilekile kilichotayarisha kibao chake kikali cha "Bailamos", Paul Barry, Mark Taylor na Brian Rawling. Video ya wimbo huu iliongozwa na Francis Lawrence.

“Rhythm Divine”
“Rhythm Divine” cover
Single ya Enrique Iglesias
kutoka katika albamu ya Enrique
Imetolewa9 Oktoba 1999 (Marekani)
MuundoCD single
ImerekodiwaAgosti-Septemba 1999
AinaLatin pop, Pop
Urefu3:30
StudioInterscope Records, Overbrook, Universal
MtunziPaul Barry na Mark Taylor
MtayarishajiMark Taylor na Brian Rawling
Mwenendo wa single za Enrique Iglesias
"Bailamos"
(1999)
"Be With You"
(2000)
Makasha badala
Kasha ya Single Pt. 2
Kasha ya Single Pt. 2

Mapokeo ya kitahikiki

Kulingana na http://www.billboard.com katika tahakiki ya single, Enrique Iglesias ameleta "ufahamu wa jitihada za kuweza kudumu kwenye chati za 40", kibao hiki ni mfano tosha kwa "wasanii wa crossover kujipatia nafasi ya kupanda ngazi ya mafanikio". Naye hufananishwa na mwimbaji mwenzake wa Kilatini Ricky Martin: "Tofauti na mwenzake Ricky Martin, Iglesias yupo mbali sana kwa kujulikana.

Orodha ya nyimbo

UK CD1
  1. "Rhythm Divine" - 3:29
  2. "Bailamos" (Eric Morillo Main Vocal Mix) - 6:30
  3. "Rhythm Divine" (Video) - 3:29
UK CD2
  1. "Rhythm Divine" (Morales Radio Mix) - 3:13
  2. "Rhythm Divine" (Fernando G Club Mix) - 5:37
  3. "Rhythm Divine" (Mijango's Extended Mix) - 6:57

Michakaliko ya chati

Kibao hiki hakikupata mafanikio kama jinsi ilivyokuwa kwa "Bailamos", hata hivyo imejikongoja na kufikia katika 50 Bora huko nchini Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Australia na Uholanzi. Toleo la Kihispania la kibao hiki, -liitwa "Ritmo Total" imeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot Latin Tracks (kwa majuma manne) na Hispania. Kibao hiki kimekwenda katika platinumu nchini Urusi kwa kuuza nakala 200,000[1].

Chati (1999)/(2000)Nafasi
iliyoshika
Australia ARIA36
Ufaransa Top 10027
Italia7
Ujeruamani Top 5036
Uholanzi20
New Zealand [2]2
Hispania1
UK Singles Chart45
US Billboard Hot 10032
US Billboard Hot Latin Tracks1
US Billboard Hot Dance Club Play4

Marejeo