Ponografia

Ponografia (kutoka neno la Kigiriki cha kisasa πορνογραφία, pornografia, ambalo linaunganisha πόρνη, pornē, yaani "kahaba" au πορνεία, porneia, yaani "ukahaba"[1]), na γράφειν, grafein, "kuandika, kutunza kumbukumbu, hata mchoro", na kumalizika ns ία, ia, yaani "hali ya, mali ya, mahali pa") ni picha au maandishi yenye lengo la kuwatia ashiki watazamaji au wasomaji.

Alama XXX inatumika mara nyingi kudokeza ponografia.
Ramani ya dunia ikionyesha uhalali na uharamu wa ponografia nchi kwa nchi (miaka 18+)      Halali      Halali kiasi      Haramu      Haijulikani vizuri

Katika utandawazi ponografia inatumia njia zote za mawasiliano na kuenea katika kila pembe ya dunia, ikiathiri hasa vijana na watoto na kuchangia ubakaji na matatizo mengine[2].

Ndiyo sababu katika nchi mbalimbali kuna sheria ambazo zinaidhibiti au kuikataza na kuiadhibu kabisa, hasa inapohusisha watoto.

Pamoja na sheria, upinzani unatokana na wanaopigania haki za wanawake[3][4][5][6][7][8] na wanaofuata dini.[9][10]

Kwa mfano, Kanisa Katoliki linakataza ponografia tangu Karne za Kati, na katika Katekisimu yake rasmi ya sasa inaipinga tena katika n. 2354[11]

Ingawa ponografia ina madhara kwa afya ya nafsi [12], ni vigumu kuizuia kwa kuwa inagusa silika ya watu na ni biashara kubwa kabisa inayolenga pesa, si maendeleo ya jamii, na kudhalilisha binadamu. Huko Marekani tu inazungusha dola bilioni 2.5 kwa mwaka.

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: