Pambo wa jangwani

Pambo wa jangwani (kwa Kigiriki: Όσιος Παμβώ; kwa Kiarabu-Kikopti: موا au بيموا, Pemwah au Bemwah; alifariki 375 hivi) ni kati ya Wakristo wa Misri waliokwenda kuishi jangwani chini ya Antoni Mkuu[1]. Baadaye alianzisha monasteri nyingi.[2]

Mt. Pambo wa Nitria.

Alijulikana kwa hekima yake akaombwa shauri na wengi, wakiwemo Athanasius, Melania Mzee na Rufinus.

Kati ya wanafunzi wake wamo Pishoy na Yohane Mbilikimo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai au 18 Julai[3][4][5].

Misemo yake

Misemo yake katika tafsiri ya Kiswahili inapatikana ndani ya kitabu:

  • Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000ISBN 0-264-66350-0

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.