Nation of Islam

Nation of Islam (Kiarabu: أمة الإسلام‎, hufupishwa kama NOI) ni shirika la Kiislamu lenye harakati za kidini ambalo lilianzishwa mjini Detroit, Marekani, na Wallace D. Fard Muhammad tarehe 4 Julai, 1930.[2] Malengo yake hasa ni kuboresha imani za kiroho, mtima, jamii na hali za kiuchumi za Wamarekani Weusi Waislamu wa Marekani na masuala mengine ya kibinadamu.[3] Watahakiki wamelipa jina shirika kama kikundi cha mamlaka ya watu weusi, yaani, kama kikundi cha kuchochea chuki dhidi ya watu wasio weusi na Kikundi kisichowapenda Wayahudi,[4][5][6] na NOI hutazamwa kama kikundi cha chuki na kituo cha Southern Poverty Law Center.[7]

Nation of Islam
UfupishoNOI
Wito"Haki au Vinginevyo!"
MwanzilishiWallace Fard Muhammad
LimeanzishwaDetroit, Michigan, U.S.
AinaHarakati za kidini na kisiasa
Hali ya kisheriaInafanyakazi
Makao MakuuMosque Maryam, Chicago, Illinois
Mahali
TanzuAmerican Society of Muslims
Fruit of Islam
wavutinoi.org

Gazeti lake rasmi ni The Final Call. Nation of Islam halichapishi idadi halisi ya wanachama wake; mwaka wa 2007, wanachama wao walikadiriwa kufikia kati ya 20,000 na 50,000.[1]

Baada ya kutoweka kwa Fard mnamo Juni 1934, Nation of Islam liliongozwa na Elijah Muhammad, ambaye alianzisha mahali mbalimbali pa kuabudia ambapo alipaita (Mahekalu au Misikiti), shule iliyoitwa Muhammad University of Islam, mabiashara, mashamba, na mashamba makubwa na ujenzi wa majengo ambayo yalikuwa Marekani na nje ya Marekani.[8] Wakati wa uongozi wa Elijah Muhammad, kulikuwa na makundi kibwena, yaani, mivutano baina ya watu hawa na wale hadi kupelekea kuondoka kwa kiongozi mkubwa katika shirika Bwana Malcolm X na kuamua kuwa dhehebu la Sunni. Baada ya kifo cha Elijah Muhammad mnamo 1975, mtoto wake Warith Deen Mohammed kabadili jina la jumuia na kuliita "World Community of Islam in the West" (na mara mbili baada ya hapo), na baadaye alijaribu kulirudisha shirika katika muundo mkuu wa Kiislamu wa itikadi za Kisunni.

Mwaka wa 1977, Louis Farrakhan alikataa uongozi wa Warith Deen Mohammed na kuainzisha upya Nation of Islam katika misingi ya awali. Kachukua hekalu ya makao makuu ya Nation of Islam, Mosque Maryam (Mosque #2), ambalo lipo Chicago, Illinois. Tangu 2010, chini ya Farrakhan, wanachama wanaonekana kuzidi.[9]

Wanachama wanaojulikana wa sasa na wa awali

Elijah Muhammad
  • Elijah Muhammad
  • Tynetta Muhammad
  • Louis Farrakhan
  • Khalid Abdul Muhammad
  • Khadijah Farrakhan
  • Malcolm X – baadaye kabadili na kuwa Sunni Islam
  • Muhammad Ali – kabadili na kuwa Sunni mnamo 1975, na Sufism mnamo 2005[10]
  • Mustapha Farrakhan – Nahodha Mkuu wa Nation of Islam
  • Mustapha Farrakhan, Jr. - mchezaji mpira wa kikapu wa kulipwa
  • Wesley Muhammad – mwanahistoria na profesa
  • Warith Deen Mohammed – baadaye kabadili na kuwa Sunni
  • Clarence 13X – baadaye kaanzisha Nation of Gods and Earths
  • Jay Electronica – msanii wa hip-hop na mtayarishaji wa rekodi
  • MC Ren – baadaye kabadili na kuwa Sunni[11]
  • Kam – mwanachama wa Nation of Islam na mshirika wa zamani wa Ice Cube
  • John Allen Muhammad – Askari mstaafu wa vita ya Ghuba, na mwanachama wa zamani wa NOI, mkosefu wa mashambulizi ya Wadunguaji wa Beltway[12]
  • Benjamin Chavis Muhammad
  • Paris –
  • Snoop Dogg[13] – baadaye kabadili kaenda imani ya Rastafari.
  • Quanell X – mwanachama tangu miaka ya 1990 - 2001, sasa ni mwanachama wa New Black Panther Party
  • David Muhammad – kiongozi wa kitaifa wa Trinidad na Tobago
  • Humza Al-Hafeez – mwanzilishi wa Jumuia ya Kitaifa ya Polisi Wamarekani Weusi, mwandishi, mwanaharakati wa kijamii wa Kimarekani
  • Shahrazad Ali – mwandishi

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons