Nash Aguas

Mwigizaji

Nash Aguas (alizaliwa kama Aeign Zackrey Aguas tarehe 10 Oktoba 1998) ni mwigizaji wa filamu na televisheni kutoka nchini Ufilipino. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama Peping katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Kifilipino maarufu kama Gulong ng Palad, Kwa sasa anahudumu kama Diwani wa Jiji la Cavite tangu tarehe 30 Juni 2022.

Nash Aguas

AmezaliwaAeign Zackrey Aguas
10 Oktoba 1998 (1998-10-10) (umri 25)
Jiji la Cavite, Ufilipino
Kazi yakeMwigizaji
Mwanasiasa
Miaka ya kazi2004–hadi leo

Wasifu

Nash alianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye televisheni, ni baada ya kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mkali wa MTB kupitia Batang F4. Aliingia rasmi katika shughuli za uigizaji ni baada ya kujiunga katika mashindano ya kipinid cha TV cha kutafuta watoto wenye vipaji vya uigizaji cha ABS-CBN maarufu kama Star Circle Kid Quest, ambamo alijiigiza kama Mr. Suave Mdogo.

Alionyesha uwezo na uchangamfu mkubwa na kupelekea kupata kura za Bibbo Kid Of The Week mara kedekede. Kitendo cha kuwa na uwezo, yaani (kipaji, maarifa, mwonekano, na ucheshi wake), kumemfanya ashinde taji la Grand Kid Questor na pia kuchukua zawadi maalum kibao katika maonyesho ya vipindi.

Filamu

Televisheni

MwakaJinaJina aliliotumiaMtandao
2004Star Circle Questkama jina lake/mshindaniABS-CBN
Mga Anghel Na Walang LangitABS-CBN
2005Gulong ng PaladPepingABS-CBN
2005-presentGoin' Bulilitkama jina lakeABS-CBN
2006Calla LilyTerrenceABS-CBN
Komiks Presents: Vulcan 5BoyetABS-CBN
Komiks Presents: Inday sa BalitawBoyongABS-CBN
2007Maria FlordelunaReneboy AlicanteABS-CBN
Sineserye Presents: Natutulog Ba Ang Diyos?Mark mdogoABS-CBN
2008LoboTikboyABS-CBN

Filamu za kawaida

MwakaJinaJina alilotumiaKampuni
2005Hari ng SablayJay-jay
Happily Ever AfterLeeboy
2006Shake, Rattle & Roll 8: "Yaya"BenjoRegal Films
2007Shake, Rattle and Roll 9: "Christmas Tree"StephenRegal Films
Angels
TiyanaksBiboy
2008DayoSauti ya Bubuy
2009[1]Land Down UnderTBA

Muziki

Albamu ya Dansi

  • Jump Around: Albamu ya Dansi ya Watoto ya Moose Gear

Tuzo

  • 2006 Metro Manila Film Festival, Mwigizaji Bora wa Kitoto kwa kucheza katika Shake, Rattle & Roll 8: "Yaya" [2]

Marejeo

Viungo vya Nje