Mto Marne unaanza katika platuu ya Langres, unatiririka kuelekea kaskazini, kisha unaelekea magharibi kati ya Saint-Dizier na Châlons-en-Champagne, na kuungana na Seine katika Charenton katika Paris.Katika kanda la Champagne sehemu ya maji huongozwa katika ziwa la kujengwa na binadamu la Lac du Der-Chantecoq, ili kudhibiti mtiririko wa maji. Kwa njia hiyo kiwango cha maji cha chini huzuiwa.[2]
Mto Marne ulikuwa eneo la mapigano mawili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. La kwanza Lilikuwa mgeuko wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika mwaka wa 1914. La pili lilitokea miaka minne baadaye, katika mwaka wa 1918.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Marne kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.