Mozaiki (au mosaiki) ni mtindo wa pekee wa uchorajipicha unaotumia vipande vidogo vya kioo cha rangi au vijiwe au vigae vya rangi mbalimbali vinavyounganishwa kuwa picha. Kunawezekana pia kutumia vipande vya vitu vyovyote vyenye rangi vinavyoweza kuunganishwa kuwa picha.
Mtindo huu ulionekana mara ya kwanza huko Phrygia (katika Uturuki ya leo) iliyokuwa sehemu ya ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. Mawe ya rangi nyeupe na nyeusi yalipangwa ukutani au kwenye sakafu kuwa tarakibu.
Baadaye Wagiriki na zaidi Waroma waliendelea kuongeza rangi na kutunga picha kamili si tarakibu tu kwenye kuta za nyumba. Maghofu ya Kiroma yanaonyesha mifano mingi iliyodumu hadi leo.
Sanaa ya mozaiki iliendelezwa katika ustaarabu wa Bizanti. Wabizanti walipamba makanisa, majumba ya kifalme na pia nyumba za matajiri kwa mozaiki nzuri kabisa.
Waarabu Waislamu walipotwaa shemu kubwa za milki ya Bizanti waliendelea kuwaajiri wasanii Wabizanti wakipamba misikiti kama msikiti wa Umawiya huko Dameski au majumba ya masultani.
Baadaye walikuwa mafundi Waislamu waliopamba makanisa na nyumba katika Italia ya kusini.
Mtindo wa mozaiki umeaendelea kutumiwa hadi leo. Kwa kawaida mozaiki inaendelea kuwa picha inayounganishwa kwa njia ya kudumu na ukuta au safau ya jengo fulani. Inawezekana pia kuifunga katika fremu na kubadilisha mahali pake lakini picha za mozaiki huwa nzito.
Lowden, John. Early Christian and Byzantine art. Phaidon.(for the section of Byzantium and Sicily)
Efthalia Rentetzi, stylistic relationships between the mosaic flooring of s. Maria delle Grazie and s. Eufemia in Grado.An unknown picture of a fish, in [1], Art on web, punti di vista sull'arte.
Efthalia Rentetzi, Un frammento inedito di S. Eufemia a Grado. Il pavimento musivo del Salutatorium", in: [2]Archived 4 Aprili 2010 at the Wayback Machine., Arte Cristiana, n. 850 (Gennaio - Febbraio 2009), V.XCVII, pp. 51–52.
Efthalia Rentetzi, Le influenze mediobizantine nei mosaici dell’arcone della Passione della Basilica marciana, in “Arte|Documento”, vol. XIV, (2000), pp. 50–53.
Makala hiyo kuhusu "Mozaiki" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.