Monie Love

Simone Gooden (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Monie Love; amezaliwa 2 Julai 1970) ni emcee kutoka nchini Uingereza na mtangazaji wa redio wa zamani huko nchini Marekani.

Monie Love
Jina la kuzaliwaSimone Gooden
Pia anajulikana kamaMonie Love
Amezaliwa2 Julai 1970 (1970-07-02) (umri 54)
Asili yakeLondon, England
Aina ya muzikiHip hop
BritHop
New jack swing
Kazi yakeRapa, mwimbaji wa hip hop
Miaka ya kazi1989–hadi sasa
StudioWarner Bros. Records
Cooltempo/Chrysalis/EMI Records
Tuff Groove
Ame/Wameshirikiana naNative Tongues
Dave Angel

Alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika hip hop ya Kiingereza, na kuleta mgongano/athira kubwa na wasaili/maemcee wengine wa kike wa Kimarekani kama vile Queen Latifah, vilevile kupitia uanchama wake na baadhi ya makundi mwishoni mwa miaka ya 1980/mwanzoni mwa miaka ya 1990 - Native Tongues. Love alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza wa BritHop kuingia mkataba na kusambaziwa kazi zake dunia nzima na mastudio makubwakubwa duniani.

Miaka ya awali

Love alizaliwa katika eneo la Battersea la mjini London. Huyu ni mdogo wake mwnamuziki wa muziki wa techno Dave Angel, na alikuwa binti wa baba aliyekuwa akipiga muziki wa jazz kutoka mjini London.

Shughuli za muziki

Love alizanza kazi yake ya hip hop/BritHop akiwa kama emcee kwenye kundi la Kiingereza la Jus Bad, kundi ambalo linaunganishwa na DJ Pogo, Sparki, na MC Mell'O'. Kundi hilo lilitoa kibao cha kilichokwenda kwa jina la "Free Style/Proud" katika studio moja ya kujitegemea Tuff Groove mnamo 1988.

Love alianza kujipatia umaarufu wake wa kujulikana kibiashara nchini Marekani baada ya kuuza sura katika single ya Queen Latifah iliyojishindia Grammy Award "Ladies First," vilevile kwenye kibao cha Adeva "Ring My Bell," na kwa kina Jungle Brothers' "Doin' Our Own Dang," na kibao kikali cha kina De La Soul "Buddy." Umaarufu huo umepelekea kuingia mkataba na Warner Bros. Records, inamfanya Love kuwa miongoni mwa wasanii wachacha sana wa British hip-hop kufanya juhudi za kutoa kazi zao na mastudio makubwakubwa duniani.

Diskografia

Albamu zake

MwakaJinaNafasi ya chati
U.S.U.S. R&B
1990Down to Earth10926
1993In a Word or 275

EP/Single alizofanya akiwa kivyake

Maelezo ya Albamu
Slice Of Da Pie EP
  • Imetolewa: 2 Mei 2000
  • Nafasi ya chati:
  • RIAA certification:

Single Alizoshirikishwa

Marejeo

Viungo vya nje

Kigezo:Monie Love