Mikoa ya Italia

Mikoa ya Italia ni vitengo vikuu vya utawala chini ya ngazi ya taifa nchini. Eneo lote la Italia limegawiwa katika mikoa 20. Kila mkoa huwa na kiwango cha madaraka cha kujiamulia, lakini mikoa 5 huwa na madaraka ya kujitawala. Madaraka hayo na kuwepo kwa kila mkoa yameandikwa katika katiba ya nchi.

Mikoa ya Italia (nyekundu: mikoa ya kujitawala)

Kila mkoa - isipokuwa ule wa Bonde la Aosta - hugawiwa katika wilaya.

Madaraka ya mikoa ya kawaida na mikoa ya kujitawala

Kikatiba kila mkoa huwa na madaraka ya kujiamulia kuhusu mambo pasipo sheria ya kitaifa na katika mambo yafuatayo:

Mikoa mitano ya kujitawala huwa na madaraka makubwa zaidi yanayotofautiana kati ya mkoa na mkoa. Sababu za haki hizo za pekee ni za kihistoria na kuwepo kwa sehemu za wananchi wenye lugha mama tofauti na Kiitalia. Mikoa hii ni Bonde la Aosta (Kiitalia-Kifaransa), Friuli-Venezia Giulia (Kiitalia-Kifurlan-Kislovenia), Sardinia (Kisardinia), Sisili na Trentino-Alto Adige/Südtirol (Kiitalia - Kijerumani).

Mikoa hii inaitwa "mikoa yenye sheria za pekee"; kwa mfano Friuli-Venezia Giulia inabaki na asilimia 60 za kodi kutoka eneo lake, Sardinia na 70%, Trentino-Alto Adige/Südtiro pamoja na Aosta zinashika 90% na Sisili inashika kodi zote chini ya mamlaka ya kimkoa.

Orodha ya mikoa

BenderaJinaMakao makuuEneo (km2)WakaziMsongamano wa watu/km²WilayaMijiMiji mikubwaHali ya utawala
AbruzzoL'Aquila10,7631,307,9191224305-Kawaida
Bonde la AostaAosta3,263126,93339074-Kujitawala
ApuliaBari19,3584,045,9492096258BariKawaida
BasilicataPotenza9,995575,902582131-Kawaida
CalabriaCatanzaro15,0811,954,4031305409Reggio CalabriaKawaida
CampaniaNapoli13,5905,761,1554245551NapoliKawaida
Emilia-RomagnaBologna22,4464,354,4501949348BolognaKawaida
Friuli-Venezia GiuliaTrieste7,8581,219,3561554218TriesteKujitawala
LazioRome17,2365,550,4593225378RomeKawaida
LiguriaGenoa5,4221,565,3492894235GenoaKawaida
LombardiaMilan23,8619,749,593409121544MilanKawaida
MarcheAncona9,3661,541,6921655239-Kawaida
MoliseCampobasso4,438312,394702136-Kawaida
PiemonteTurin25,4024,366,25117281206TurinKawaida
SardiniaCagliari24,0901,637,193688377CagliariKujitawala
SisiliaPalermo25,7114,994,8171949390Catania, Messina, PalermoKujitawala
Trentino-Alto Adige/SüdtirolTrento13,6071,036,707762333-Kujitawala
ToscanaFirenze22,9943,679,02716010287FirenzeKawaida
UmbriaPerugia8,456885,535105292-Kawaida
VenetoVenisi18,3994,865,3802647581VenisiKawaida