Michelle Rodriguez

Mwigizaji wa Marekani

Mayte Michelle Rodriguez[1] alizaliwa 12 Julai 1978[2] anayejulikana kuigiza filamu kama Girlfight, The Fast and The Furious, Blue Crush, Resident Evil, S.W.A.T., na Avatar. Vilevile, ameigiza kama Ana Luzia Cortez kwenye kipindi cha Lost.

Michelle Rodriguez
Rodriguez mnamo 2013
Rodriguez mnamo 2013
Jina la kuzaliwaMayte Michelle Rodríguez
Alizaliwa12 Julai 1978
Marekani
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi1999 - hadi leo
WazaziCarmen Milady,
Rafael Rodriguez
Tovuti Rasmi michelle-rodriguez.com

Maisha yake

Rodriguez alizaliwa mjini Bexar County, Texas. Yeye ni mtoto wa Carmen Milady na Rafael Rodriguez - aliyefanya kazi kwa jeshi la Marekani.[3]Rodriguez alihamia nchini Dominican Republic alipokuwa na miaka minane pamoja na mamake na akaishi Puerto Rico mpaka alipofika miaka kumi na moja, na baadaye kuhamia mjini New Jersey. Rodriguez alijiunga na chuo kikuu na kusomea biashara lakini akaiacha na kujiunga na shule ya uigizaji, akiwa na azma ya kuwa mwandishi wa filamu.[4]

Uigizaji

Rodriguez kwenye sherehe ya New York Fashion Week mnamo 2006
Filamu
MwakaFilamuAliigiza kamaMaelezo
2000GirlfightDiana Guzman
2001The Fast and the FuriousLetty
3 A.M.Salgado
2002Blue CrushEden
Resident EvilRain Ocampo
2003S.W.A.T.Chris Sanchez
2004ControlTeresa
2005BloodRayneKatarin
2006The BreedNicki
2007Battle in SeattleLou
2008A Cat's TaleJujubeSauti
Gardens of the NightLucy
2009Fast & FuriousLetty
Trópico de SangreMinerva Mirabal
AvatarTrudy Chacon
2010MacheteLuz
2011Battle: Los AngelesCorporal Adriana Santos
Army of TwoAlice Murray
2012Resident Evil: RetributionRain Ocampo
Filamu
MwakaJinaAliigiza kamaVipindi
2005Punk'dMwenyewe1
Immortal Grand PrixLiz Ricarro26
2005-2006, 2009LostAna Lucia Cortez25
2007Adventures in Voice ActingMwenyewe1

Mashtaka

Mnamo Machi 2002, Rodriguez alifungwa kwa ajili wa kumpiga rafiki yake.[5] Madai haya yalitolewa pindi aliyempiga alipokataa kwenda kutoa ushahidi mahakamani.[6]Mnamo Juni 2004, Rodriguez alishtakiwa kwa kuendesha gari ilhali alikuwa amelewa.[7] Alipelekwa rumande kwa masaa 48.

Mnamo 2005, alipokuwa anarekodi Lost mjini Hawaii, alishikwa mara kadhaa na polisi kwa ajili ya kuvunja sheria barabarani na akatozwa faini ya $357.[8]

Maisha ya kibinafsi

Mnamo 2000, alipendana na Muislamu lakini akaachana naye akisema kuwa dini hiyo ina sheria nyingi.[9] Mnamo 2003, Rodriguez ameonekana akiwa na muigizaji Olivier Martinez nchini Ufaransa.[10]

Marejeo