Michelangelo
(Elekezwa kutoka Michelangelo Buonarroti)
Michelangelo di Lodovico Buonarroti Simoni (6 Machi 1475 - 18 Machi 1564) alikuwa msanii nchini Italia aliye maarufu kama mchongaji, mchoraji, msanifuujenzi na mshairi. Huhesabiwa kati ya wasanii muhimu zaidi wa zama ya mwamko.
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/5e/Miguel_%C3%81ngel%2C_por_Daniele_da_Volterra_%28detalle%29.jpg/200px-Miguel_%C3%81ngel%2C_por_Daniele_da_Volterra_%28detalle%29.jpg)
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/63/Michelangelos_David.jpg/220px-Michelangelos_David.jpg)
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/8e/Michelangelo_-_Fresco_of_the_Last_Judgement.jpg/220px-Michelangelo_-_Fresco_of_the_Last_Judgement.jpg)
Kati ya kazi zake maarufu zaidi ni sanamu ya kijana Daudi na michoro ya ukutani wa Kikanisa cha Sisto IV huko Vatikano mjini Roma alichopamba kwa hadithi na watu wa Biblia.
Kati ya kazi zake maarufu kama msanifuujenzi ni hasa kuba ya Basilika la Mt. Petro kwenye Vatikano mjini Roma.
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Picha
- Yesu awekwa kaburini, mafuta juu ya ubao, 161 × 149 cm
- Mateso ya Mt. Petro, Kanisa Paolina - Vatikano.
- Familia Takatifu na mtoto Yesu (Iko Firenze)
- Mtumwa anayekufa
- Bacchus (mungu wa Kiroma)
- Sanamu ya Musa (Vatikano)
- Kuba ya Basilika la Mt. Petro katika Vatikano ilitungwa na Michelangelo
![]() | Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michelangelo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaMikoa ya TanzaniaShairiOrodha ya makabila ya TanzaniaKisaweMtumiaji:MsafiriOrodha ya Marais wa MarekaniTanzaniaMadawa ya kulevyaMpira wa miguuKumaHaki za watotoSimba S.C.Orodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliTendo la ndoaLawrence Kego MashaHistoria ya TanzaniaOrodha ya Watakatifu WakristoAina za manenoDonald TrumpMaumivu ya kiunoOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaLilithUkimwiOrodha ya vitabu vya BibliaDiamond PlatnumzVichekeshoJean BalekeUsafi wa mazingiraVivumishiJumuiya ya Afrika MasharikiSentensiMazingiraBendera ya Kenya