Mbwana Samatta

Mchezaji wa chama cha soka Tanzania

Mbwana Ally Samatta, (alizaliwa 23 Disemba 1992), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania katika klabu ya Feberbahce nchini Uturuki [1]. Mbwana ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akucheze timu ya Aston Villa nchini Uingereza[2].

Mbwana Samatta
Maelezo binafsi
Jina kamiliMbwana Aly Samatta
tarehe ya kuzaliwa23 Desemba 1992 (1992-12-23) (umri 31)
mahali pa kuzaliwaDar es Salaam, Tanzania
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasaFenerbahce
Youth career
2008–2010African Lyon
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2010–2011Simba
2011–2016TP Mazembe
2016–2020K.R.C Genk
2020– 2020Aston Villa
Timu ya Taifa ya Kandanda
Tanzania17(6)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 24 March 2013

Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba S.C. mwaka 2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.

Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].

Kazi

Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]

Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[6]

Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8]

Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).

Maisha binafsi

Mbwana Samatta ni Mndengereko kutoka Kibiti kwa kabila. Katika maisha ya imani ni Muislamu.[9]

Takwimu za michezo

Klabu

Michezo na magoli ya klabu, Msimu na mashindano
KlabuMsimuLigiCupKombe la ligiYa BaraMengineyoJumlaRef.
UshindaniMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoliMichezoMagoli
Simba S.C.2010–11Ligi Kuu Tanzania Bara2513Kigezo:Efn22515[10][11]
TP Mazembe2011Linafoot8282[10][11]
20122923963729[10][11]
201337205Kigezo:Efn54225[10][11]
2013–142915843719[10][11]
2014–156464[11]
2015–166464[11]
Jumla103600033230013683
K.R.C. GenkLigi kuu ya Ubelgiji620012Kigezo:Efn3185[12]
2016–1727104218510Kigezo:Efn35920[12]
2017–182044011Kigezo:Efn4358[12]
2018–1928201012910Kigezo:Efn35132[12]
Jumla813692003014431316365
Jumla maisha ya soka209109920063394313324163

Kimataifa

[10]

Taifa Stars
MwakaMichezoMagoli
201192
201240
2013106
201431
201572
201641
201733
201852
201961
Total5118

Magoli Kimataifa

GoliTareheUwanjaMpinzaniAlamaMatokeoMashindano
1.26 Machi 2011Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania  Jamhuri ya Afrika ya Kati2–12–1kufuzu AFCON 2012
2.3 Septemba 2011  Algeria1–01–1
3.11 Januari 2013Uwanja wa Adis ababa, Addis Ababa, Ethiopia  Ethiopia1–11–2Mchezo wa Kirafiki
4.6 Februari 2013Uwanja wa Taifa Dar es Salaam  Kamerun1–01–0
5.24 Machi 2013  Moroko2–03–1kufuzu fainali za kombe la dunia 2014
6.3–0
7.4 Disemba 2013Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya  Burundi1–01–0hatua ya makundi mashindano ya CECAFA 2013
8.12 Disemba 2013uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya  Zambia1–11–1mashindano ya CECAFA hatua ya mtoano 2013
9.3 Agosti 2014uwanja wa Estádio do Zimpeto, Maputo, Msumbiji  Msumbiji1–11–2Kufuzu AFCON 2015
10.7 Oktoba 2015Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania  Malawi1–02–0kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 hatua ya kwanza
11.14 Novemba 2015  Algeria2–02–2kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 – hatua ya pili
12.23 Machi 2016uwanja wa Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya, N'Djamena, Chad  Chad1–01–0kufuzu AFCON 2017 hatua ya makundi
13.25 Machi 2017Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania  Botswana1–02–0Mchezo wa kirafiki
14.2–0
15.10 Juni 2017  Lesotho1–01–1kufuzu AFCON 2019 Kundi L
16.27 Machi 2018  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo1–02–0Mchezo wa kirafiki
17.16 Oktoba 2018  Cabo Verde2–02–0kufuzu AFCON 2019
18.27 Juni 2019uwanja wa 30 June Stadium, Cairo, Misri  Kenya2–12–3AFCON 2019 Kundi C
19.8 Septemba 2019Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania  Burundi1–01–1 (3–0 mikwaju ya penalti)kufuzu michano ya kombe la dunia 2022 hatua ya kwanza

Heshima

TP Mazembe[13]

  • Linafoot: 2011, 2012, 2013, 2013–14
  • DR Congo Super Cup: 2013, 2014
  • Klabu bingwa Afrika: Klabu bingwa Afrka 2015[14][15]

Genk

  • Ligi kuu ya Ubelgiji: msimu wa 2018–19[16]
  • Belgian Super Cup: michuano ya pili ya Ubelgiji 2019[17]

Binafsi

  • Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika: 2015
  • Timu yam waka ya CAF: 2015[18]
  • Mfungaji bora ligi ya mabingwa Afrika: 2015[4]
  • Mchezaji bora ligi ya Ubelgiji: 2019[3]
  • Mfungaji bora ligi ya Ubelgiji: msimu wa 2018-19[17]

Marejeo

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbwana Samatta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.