Malibu's Most Wanted

Malibu's Most Wanted ni filamu ya vichekesho ya mwaka wa 2003 ambayo imetungwa na kuchezwa na Jamie Kennedy akiwa na washiriki wenzi Taye Diggs, Anthony Anderson, na Regina Hall.

Malibu's Most Wanted
Imeongozwa naJohn Whitesell
Imetayarishwa naFax Bahr
Mike Karz
Adam Small
Imetungwa naFax Bahr
Adam Small
Jamie Kennedy
Nick Swardson
NyotaJamie Kennedy
Taye Diggs
Anthony Anderson
Blair Underwood
Regina Hall
Damien Dante Wayans
Jeffrey Tambor
Pamoja na Bo Derek
Na Ryan O'Neal
Muziki naJohn Debney
John Van Tongeren
Imesambazwa naWarner Brothers
Imetolewa tar.10 Aprili 2003
Ina muda wa dk.86 min.
LughaKiingereza
Bajeti ya filamu$15 million
Mapato yote ya filamu$34,622,504[1]

Filamu hii ilitungwa na waanzilishi wa MADtv, Fax Bahr na Adam Small, ambao pia wamesimama kama watayarishaji wa filamu hii.

Uhusika wa "B-Rad" awali ulionekana kipindi cha kujificha kwenye kamera cha Jamie Kennedy, The Jamie Kennedy Experiment, lakini ilianza tangu enzi zake za ucheshi wake wa wima na kuufanya kama utaratibu endelevu.

Hadithi

Filamu inaanza katika maisha ya familia ya Bill Gluckman, seneta Myahudi Mzungu kutoka mjini Malibu, California ambaye anagombea Ugavana wa California. Mtoto wake Brad ni Wigger (Wigger ni nadharia ya mtu Mzungu anayefuata tabia au tamaduni za Wamarekani Weusi - hasa katika hip hop), amejipendekeza mwenyewe jina la utani la "B-Rad" licha ya kuwa na utajiri katika familia yake, maisha ya kivulini. Imetokea, wanachama wa Bwana Gluckman wa kampeni za kisiasa wamekuwa na wasiwasi na upuuzi wa Brad, tabia za kishenzi zinazopelekea kuharibu nafasi ya baba'ke asichaguliwe.

Wanachama wa kikosi cha kampeni kimekodisha waigizaji wawili, ambao hawajui undani zaidi wa maisha ya mjini zaidi ya B-Rad, kwa kuigiza kama majambazi, wakamtekanyara, na wakampeleka huko South Central Los Angeles ambapo walitumainia kwamba Brad ataogopa kwa kuwa yeye mzungu - hasa baada ya kushuhudia maisha ya kitaa yapo vipi. Kwa bahati mbaya kila aliyejiingiza, mpango unavurugika baada ya Brad kutaka kujihusisha na vikundi vya kihuni na baadaye akajiingiza mwenyewe na wale waigizaji waliotumwa kuja mzingua nao pia wanamwongoza pabaya.

Washiriki

MwigizajiUhusika
Jamie KennedyBrad "B-Rad G" Gluckman
Taye DiggsSean
Anthony AndersonPJ
Regina HallShondra
Blair UnderwoodTom Gibbons
Damien Dante WayansTec
Ryan O'NealBill Gluckman
Bo DerekBess Gluckman
Jeffrey TamborDr. Feldman
Kal PennHadji
Nick SwardsonMocha
Keili LefkovitzMonster
Kellie MartinJen
Greg GrunbergBrett
J. P. ManouxGary
Terry Crews8 Ball

Walionekana

  • Snoop Dogg (sauti ya panya)
  • Mike Epps (DJ kule klabu)
  • Felli Fel
  • Hi-C
  • Young Dre The Truth
  • Drop da Bomb
  • Hal Fishman
  • Big Boy

Marejeo

Viungo vya Nje