Liz McDaid

Liz McDaid ni mwanaharakati wa Afrika Kusini ambaye ni kiongozi wa "Eco-Justice" wa Taasisi ya Mazingira ya Jumuiya za Kiimani Kusini mwa Afrika (SAFCEI).[1].Pamoja na Makoma Lekalakala, alitunukiwa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo mwaka 2018 kwa eneo la Afrika kwa kazi yao ya kutumia mahakama kusitisha makubaliano ya nyuklia ya Urusi na Afrika Kusini mnamo mwaka 2017.[2]Mnamo mwaka 2018 McDaid na Lekalakala walipokea Tuzo ya Ukumbusho ya Nick Steele kwa kushinda kesi muhimu ya korti ya kusitisha mipango ya serikali ya Afrika Kusini kuendelea na mpango wa kitaifa wa ujenzi wa nyuklia.

Marejeo