Kuvuja damu baada ya kuzaa

Kuvuja damu baada ya kuzaa au kutokwa na damu baada ya kuzaa (PPH) mara nyingi hufasiliwa kama kupoteza zaidi ya mililita 500  au 1,000  za damu ndani ya saa 24 za baada ya kuzaa.[1] Baadhi ya watu wameongeza hoja kwamba lazima mtu awe na dalili za upungufu wa kiwango cha damu ili hali hii itambulike kuwepo.[2] Ishara na dalili mwanzoni zinaweza kujumuisha: ongezeko la mapigo ya moyo, kuhisi kizunguzungu baada ya kusimama na ongezeko la kiwango cha pumzi.[3] Kwa sababu kiwango kikubwa zaidi cha damu hupotea, mwanamke huyu anaweza kuhisi kijibaridi, shinikizo lake la damu linaweza kupungua na anaweza kuanza kuhangaika au kupoteza ufahamu.[3] Hali hii inaweza kutokea hadi wiki sita baada ya kuzaa.[2]

Kuvuja damu baada ya kuzaa
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyObstetrics Edit this on Wikidata
ICD-10O72.
ICD-9666
eMedicinearticle/275038
MeSHD006473

Kisababishi

Kisababishi kikuu cha hali hii ni mikazo hafifu ya uterasi kufuatia kuzaa. kukosa kutolewa kwa plasenta yote, kuraruka kwa uterasi, au hali duni ya kuganda kwa damu ni hali zingine zinazoweza kuwa visababishi. Hali hii hutokea mara nyingi katika watu ambao: tayari wana kiwango cha chini cha seli nyekundu za damu, ni mtu wa bara Asia, watu walio na watoto wakubwa zaidi au zaidi ya mtoto mmoja, wanene kupindukia au wa umri wa zaidi ya miaka 40. Hali hii pia hutokea mara nyingi baada ya kuzaa kwa njia ya upasuaji, katika wanawake ambao hupewa dawa ili waanze kupata mikazo ya kuzaa, au wanawake walio na episiotomia.[1]

Kinga na matibabu

Kinga hujumuisha kupunguza vipengele vinavyojulikana vya hatari ikiwa ni pamoja na, ikiwezekana, taratibu zinazohusiana na hali hii na kupeana dawa ya oxytocin ili kusisimua uterasi ukazike punde baada ya mtoto kuzaliwa. Misoprostol inaweza kutumika badala ya oxytocin katika jamii za mapato ya chini. Matibabu yanaweza kujumuisha: maji yanayodungwa ndani ya mishipa, kuongezwa zamu na dawa ya ergotamine ili kusababisha mikazo zaidi ya uterasi. Juhudi za kukaza uterasi kwa mikono zinaweza kusaidia ikiwa njia zingine za matibabu hazisaidii. Mshipa wa aota pia unaweza kubanwa kwa kufinya fumbatio. Shirika la Afya Duniani limependekeza vazi la kuzuia mshtuko lisilotumia hewa kusaidia hadi hatua zingine kama vile upasuaji zichukuliwe.[1]

Epidemiolojia

Katika mataifa yanayostawi, takriban asilimia 1.2 ya wanawake wanaozaa hukumbwa na hali ya kuvuja damu baada ya kuzaa, na hali hii ilipotokea, takriban asilimia 3 ya wanawake walifariki.[1] Hali hii husababisha vifo 44,000 hadi 86,000 kote duniani kila mwaka, hivyo ndicho kisababishi kikubwa zaidi cha kifo katika ujauzito.[1][4] Takriban 0.4 ya wanawake 100,000 wanaozaa hufariki kutokana na kuvuja damu baada ya kuzaa katika mataifa ya Uingereza, ilhali takriban wanawake 150 kati ya 100,000 wanaozaa hufa katika mataifa ya kusini mwa jangwa sahara. Viwango vya vifo vimepungua pakubwa tangu angalau miaka ya mwisho wa 1800 katika mataifa ya Uingereza.[1]

Marejeleo