Kutabaruku

Kutabaruku (kutoka mzizi wa Kiarabu unaokazia neno la kubariki) ni tendo la kuweka wakfu kwa Mungu altare, hekalu, kanisa au jengo lingine la kidini.[1]

Kumbukumbu kwa Kilatini ya kutabaruku kwa kanisa la abasia ya Prüfening, Ujerumani.

Sikukuu ya kutabaruku

Sikukuu ya kukumbuka tarehe ya kutabaruku hekalu au kanisa fulani inafanyika tangu zamani.

Katika Biblia

Hanukkah, au "Sikukuu ya Wamakabayo", ni sikukuu ya Uyahudi inayodumu siku nane kuanzia tarehe 25 Kislev (mnamo Desemba, lakini pengine mwishoni mwa Novemba). Ilianzishwa na Yuda Mmakabayo na wenzake mwaka 165 KK kisha kutakasa Hekalu la Yerusalemu na hasa altare yake kutokana na unajisi uliosababishwa na mfalme Antioko Epifane (168 KK) alipodhulumu Uyahudi. [2] [3]

Yesu alishiriki sikukuu hiyo (Yoh 10:22) inayotajwa na Mtume Yohane kwa jina la τὰ ἐγκαίνια, ta engkainia, "the renewals").[4] Yosefu Flavio anaiita "mianga" tu.[5]

Katika Ukristo

Katika madhehebu mbalimbali, kama Kanisa Katoliki, Orthodoksi na Anglikana, makanisa yanawekwa wakfu na askofu kwa ibada inayoitwa kutabaruku.

Utaratibu mzima wa Kanisa la Kilatini unapatikana katika Caeremoniale Episcoporum, sura IX-X, na katika Missale Romanum.

Desturi hiyo ni ya kale, labda kama ujenzi wenyewe wa makanisa. Mwanzoni mwa karne ya 4 inashuhudiwa sehemu nyingi.[6]

Inawezekana sana kwamba desturi hiyo ilitokana na ile ya Agano la Kale. [7][8]

Tazama pia

  • Wakfu
  • Jiwe la msingi
  • Ex-voto

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: