Klementina Anuarite

mauaji ya Kikongo

Maria Klementina Anuarite Nengapeta[1][2] (Wamba, 29 Desemba 19391 Desemba 1964) alikuwa mtawa wa shirika la masista wa Familia Takatifu huko Bafwabaka,[3](leo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Aliuawa mwaka 1964 na Colonel Pierre Colombe, kiongozi mmojawapo wa waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoitwa Simba revolt, [4]kwa sababu alikataa kufanya naye ngono[5][6].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Agosti 1985.[7]

Ni mwanamke wa kwanza wa Kibantu kupewa heshima hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 1 Desemba.

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.