Kito (madini)
Kito (pia: johari, jiwe la thamani) ni madini adimu na ngumu zinazopendeza kwa sababu ya uangavu na rangi yake. Vito mbalimbali vinapendwa na watu na kutumiwa kama mapambo. Kito chenye ugumu na thamani kubwa ni almasi.
Mara nyingi vinakatwa, kusuguliwa na kung'arishwa kwa namna mbalimbali na kutumiwa pamoja na metali adili kama dhahabu au fedha kuwa mapambo kama pete, hereni, mkufu au bizimu.
Mifano ya vito ni
- almasi
- feruzi
- yakuti
- zumaridi
- tanzanaiti
Lulu na korali hutajwa wakati mwingine pia kama kito ingawa si minerali asilia lakini dutu inayotengenezwa na wanyama.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kito (madini) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoAina za manenoKumaShairiKamusi za KiswahiliDiamond PlatnumzMaumivu ya kiunoInsha ya wasifuSimba S.C.Fasihi simuliziIdd el HajjTanzaniaOrodha ya Watakatifu WakristoHifadhi ya mazingiraMikoa ya TanzaniaMaalum:MabadalikoyaKaribuniKisaweNembo ya TanzaniaMapenziJohn Raphael BoccoMapenzi ya jinsia mojaTendo la ndoaVivumishiUandishi wa ripotiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMazingiraMpira wa miguuMshororoVitendawiliOrodha ya makabila ya TanzaniaMadawa ya kulevyaMasoud KipanyaKiswahiliNahauMofimuVita Kuu ya Pili ya Dunia