Kipanya-misitu

Kipanya-misitu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli:Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda:Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda:Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia:Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia:Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi:Hylomyscus
Thomas, 1926
Ngazi za chini

Spishi 21:

  • H. aetus (Thonas, 1911)
  • H. alleni (Waterhouse, 1838)
  • H. anselli (Bishop, 1979)
  • H. arcimontensis Carleton & Stanley, 2005
  • H. baeri Heim de Balsac & Aellen, 1965
  • H. carillus (Thomas, 1904)
  • H. denniae (Thomas, 1906)
  • H. endorobae (Heller, 1910)
  • H. grandis Eisentraut, 1969)
  • H. heinrichorum Carleton, Banasiak & Stanley, 2015
  • H. kerbispeterhansi Demos, Agwanda & Hickerson, 2014
  • H. mpungamachagorum Demos, Hutterer & Kerbis Peterhans, 2020
  • H. pamfi Nicolas et al., 2010
  • H. parvus Brosset, Dubost & Heim de Balsac, 1965
  • H. pygmaeus Kerbis Peterhans, Hutterer & Demos, 2020
  • H. simus Allen & Coolidge, 1930
  • H. stanleyi Kerbis Peterhans, Hutterer & Demos, 2020
  • H. stella (Thomas, 1911)
  • H. thornesmithae Kerbis Peterhans, Hutterer & Demos, 2020
  • H. vulcanorum (Lönnberg & Gyldenstolpe, 1925)
  • H. walterverheyeni Nicolas et al., 2008

Vipanya-misitu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hylomyscus katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu na maeneo yenye midambi ya Afrika kusini kwa Sahara.

Maelezo

Vipanya hawa wana masikio makubwa yenye mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Urefu wa mwili ni mm 55-120, urefu wa mkia ni mm 75-175 na uzito ni g 6-42. Manyoya yao ni laini na kahawia hadi kahawianyekundu mgongoni na kijivu iliofifia tumboni.

Hukiakia usiku na wanaishi kwenye miti. Hula matunda, mbegu na wadudu.

Spishi