Kinengenenge

Ndege wadogo wa familia Zosteropidae
Kinengenenge
Kinengenenge wa Madagaska
Kinengenenge wa Madagaska
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila:Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli:Aves (Ndege)
Oda:Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu:Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia:Zosteropidae (Ndege walio na mnasaba na vinengenenge)
Bonaparte, 1853
Ngazi za chini

Jenasi 14:

  • Apalopteron Bonaparte, 1854
  • Cleptornis Oustalet, 1889
  • Dasycrotapha Tweeddale, 1878
  • Heleia Hartlaub, 1865
  • Lophozosterops Hartert, 1896
  • Megazosterops Stresemann, 1930
  • Oculocincta Mees, 1953
  • Rukia Momiyama, 1922
  • Sterrhoptilus Oberholser, 1918
  • Tephrozosterops Stresemann, 1931
  • Woodfordia North, 1906
  • Yuhina Hodgson, 1836
  • Zosterops Vigors & Horsfield, 1827
  • Zosterornis Ogilvie-Grant, 1894

Vinengenenge au manja ni ndege wadogo wa familia Zosteropidae. Wana rangi ya zeituni mgongoni na ya kijivu chini na mara nyingi rangi ya manjano na nyeupe pia, pengine nyekundu. Takriban spishi zote zina doa la mviringo kuzunguka macho. Domo lao ni jembamba lenye ncha kali na ulimi ni kama brashi ili kula mbochi. Vinengenenge hula wadudu hasa lakini mbochi na matunda pia. Hulijenga tago lao mtini na jike huyataga mayai buluu 2-4.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha