Kimetameta (kisubi)

Kimetameta
Kimetameta wa Nyuzilandi (Arachnocampa luminosa)
Kimetameta wa Nyuzilandi (Arachnocampa luminosa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila:Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli:Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini:Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda:Diptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda:Nematocera
Familia:Keroplatidae
Róndani, 1856
Ngazi za chini

Jenasi 3:

  • Arachnocampa Leach, 1815
  • Keroplatus Latreille, 1817
  • Orfelia LeConte, 1861

Vimetameta au vimulimuli ni lava wa visubi-kuvu wa familia Keroplatidae wanaotoa nuru (bio-uangazaji). Majina hayo yanaweza kutumiwa pia kutaja spishi za mbawakawa za familia ya juu Elateroidea. Visubi hao huitwa visubi-kuvu kwa sababu angalau sehemu ya chakula chao ni vikungunyanzi na spora za kuvu. Nuru wanayotoa ina shughuli ya kuvutia wadudu wengine wadogo. Vimetameta hao hawapatikani katika Afrika.

Lava wa jenasi tatu za visubi-kuvu huonyesha bio-uangazaji. Wanatoa nuru kijanibuluu[1]. Wanasuka tando zinazonata ili kukamata wadudu wadogo. Hupatikana katika mapango na mashimo ya miamba, chini ya miamba inayotokeza na katika mahali pengine panyevu panapokingwa. Licha ya lingano kwa shughuli na muonekano, mifumo ya bio-uangazaji ya jenasi tatu sio ya aina moja na inaaminika kuwa iligeuka kwa jinsi tofauti[2][3][4].

  • Jenasi Arachnocampa: spishi tano zinazopatikana tu katika Nyuzilandi na Australia. Mwanajenasi anayejulikana sana ni kimetameta wa Nyuzilandi, Arachnocampa luminosa. Lava ni mbuai na hutumia nuru yao kuchua mbuawa katika tando zao.[5].
  • Jenasi Orfelia: ina spishi moja tu, Orfelia fultoni, inayopatikana tu katika Amerika ya Kaskazini. Kama spishi za Arachnocampa lava wake hutumia nuru yao kuvutia wadudu mkia-fyatuo na wadudu wengine wadogo, lakini chakula chao kikuu ni spora za kuvu.
  • Jenasi Keroplatus: inapatikana huko Eurasia. Kinyume na Arachnocampa and Orfelia, lava wa Keroplatus hujilisha kwa spora za kuvu tu[6]. Bio-uangazaji yao inaaminika kutokuwa na shughuli na ni mabaki[2].

Picha

Marejeo