Kambu-ardhi

Kambu-ardhi
Kambu-ardhi kichwa-buluu
Kambu-ardhi kichwa-buluu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli:Aves (Ndege)
Oda:Coraciiformes (Ndege kama viogajivu)
Familia:Brachypteraciidae (Ndege walio na mnasaba na kambu-ardhi)
Jenasi:Atelornis Pucheran, 1846

Brachypteracias Lafresnaye, 1834
Geobiastes Sharpe, 1871
Uratelornis Rothschild, 1895

Spishi:Angalia katiba

Kambu-ardhi ni ndege wa familia Brachypteraciidae wanaotokea Madagaska tu. Wanafanana na viogajivu wadogo lakini hawana rangi kali, isipokuwa kichwa cha kambu-ardhi kichwa-buluu na kile cha kambu-ardhi kichwa-chekundu. Hutafuta chakula chini na hula wadudu na watambaachi. Tago lao ni kishimo ardhini. Jike huyataga mayai 1-4.

Spishi

Picha