Juvenal Habyarimana

Juvénal Habyarimana (8 Machi 1937 – 6 Aprili 1994) alikuwa rais wa pili wa Rwanda. Alitawala karibu mikaka 20 kuanzia 1973 hadi 1994. Alitoka katika jumuiya ya Wahutu akaongoza serikali iliyolenga kuzuia kurudi kwenye mamlaka kwa Watutsi ambao ni kundi kubwa la pili nchini Rwanda.

Juvénal Habyarimana

Habyarimana in 1980

Rais wa Rwanda wa pili
Muda wa Utawala
5 Julai 1973 – 6 Aprili 1994
mtanguliziGrégoire Kayibanda
aliyemfuataThéodore Sindikubwabo

tarehe ya kuzaliwa(1937-03-08)Machi 8, 1937
Ruanda-Urundi
tarehe ya kufaAprili 6, 1994 (umri 57)
Kigali, Rwanda
utaifaRwanda
chamaMRND
ndoaAgathe Habyarimana
diniKanisa Katoliki[1]

Kwa lugha ya Kinyarwanda aliitwa "Kinani" inayomaanisha "asiyeshindwa". Habyarimana alitawala kama dikteta na watazamaji hamini alidanganya katika kila uchaguzi aliosimamia.[2]

Alikufa tarehe 6 Aprili 1994 wakati ndege yake ilipigwa na makombora aliporejea Kigali kutoka majadiliano ya amani pale Dar es Salaam. Ndege hii ilimbeba pia rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.[3] Haijulikana kama makombora yalifyatuliwa na Wahutu wakali waliochukia siasa yake au na wanamgambo Watutsi wa RPF waliokuwa wamefika karibu na Kigali wakati ule.

Tukio hili lilichukuliwa na Wahutu wakali kama ishara ya kushambulia Watutsi kote Rwanda pamoja na Wahutu wasioshikamana nao na hivyo kuanzisha mauaji ya kimbari ya Rwanda.[4][5] Katika kipindi cha siku 100 zilizofuata, idadi ya Warwanda 800,000 hadi milioni 1 waliuawa.[6]

Marejeo

Viungo vya Nje