Ghuba ya Saint Lawrence

48°0′N 61°30′W / 48.000°N 61.500°W / 48.000; -61.500

Ghuba ya Saint Lawrence

Ghuba ya Saint Lawrence (kwa Kiingereza: Gulf of Saint Lawrence, kwa Kifaransa. golfe du Saint-Laurent) ni eneo la mdomo wa Mto Saint Lawrence katika Bahari Atlantiki. Hivyo ni pia sehemu ambako maji ya maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini yanaishia baharini. Mkono huu wa bahari umefungwa na nchi kavu ya Kanada pande tatu na una eneo la maji la km2 236,000.

Jiografia

Ghuba hiyo inapakana upande wa kaskazini na Rasi ya Labrador, upande wa mashariki na Newfoundland, upande wa kusini na Nova Scotia na upande wa magharibi na Rasi Gaspé na New Brunswick.

Kuna milango miwili ambako ghuba inaunganishwa na Atlantiki:

  • Mlangobahari wa Belle Isle baina ya Labrador na Newfoundland (una upana wa km 17 na kina cha m 60).
  • Mlangobahari wa Cabot baina ya Newfoundland na Kisiwa cha Cape Breton (una upana wa km 104 na kina cha m 480).

Tanbihi

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: