Fomula

Katika hisabati au sayansi fomula ni kanuni iliyoandikwa katika alama za kialjebra.

Fomula hutumia herufi au alama za pekee (kama π) badala ya maneno. Mfano rahisi wa formula ni y = x. Ikiwa x = 1, fomula y = x ingeweza kutoa taarifa kwamba x ni sawa na y, kwa hiyo, y = 1.

  • Fomula za hisabati: Fomula mashuhuri katika hisabati ni uhakiki wa Pythagoras a2 + b2=c2 inayomaanisha ya kwamba kwenye pembetatu mraba jumla ya miraba juu ya miguu inayokutana kwenye pembemraba (cathetus) ni sawa na mraba juu ya kiegema (hypotenuse, upande usiounganishwa na pembemraba).
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fomula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.