Danay García

Danay García (amezaliwa tar. 5 Julai 1984, mjini Havana, Kuba) ni mwigizaji filamu na tamthilia wa Kikuba. Kwa sasa anashiriki katika tamthilia ya Prison Break, na humu anacheza kama Sofia Lugo.

Danay García
Amezaliwa5 Julai 1984 (1984-07-05) (umri 39)
Havana, Kuba

Wasifu

Maisha na sanaa (kwa ufupi

Danay Garcia alizaliwa na kukulia mjini Havana, Kuba.[1]. Aliazna kazi za unenguaji tangu yungali na miaka kumi.[2]. Danay anajua kucheza muziki wa Ballet, Salsa, Dansi ya Kiafrika, Merengue, Belly Dansi, na Flamenco. Baadaye akaja kuwa mwanamitindo. Kwa sasa, ni mmoja kati washriki wa mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani cha Prison Break.Danay Garcia anaishi mjini Mexico City, na ana mume na watoto wawili.

Filamu alizocheza

MwakaJina la filamuJina alilotumiaMaelezo
2007From Mexico with LoveMaria
2007–2008Prison BreakSofia LugoMfululizo wa TV
2007CSI: MiamiCamille TavezMfululizo wa TV
2006DanikaMyra

Marejeo

Viungo vya Nje