Colin Salmon

Colin Salmon (amezaliwa tar. 6 Desemba, 1962) ni mwigizaji wa kutoka nchini Uingereza. Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Charles Robinson katika filamu tatu za James Bond na James "One" Shade kwenye Mfululizo wa wa filamu za Resident Evil. Kwa sasa yupo kama muhusika anayeonekana mara kwa mara kwenye, Walter Steele, katika mfululizo wa TV unaorushwa hewani na kina CW - Arrow.

Colin Salmon

Colin Salmon at Dinard British Film Festival (France)
AmezaliwaColin Salmon
6 Desemba 1962 (1962-12-06) (umri 61)
Bethnal Green, London, England, UK
Kazi yakeMwigizaji
Miaka ya kazi1992–hadi sasa
NdoaFiona Hawthorne (1988-present)
[miley.co.uk/colinsalmon/index.html Tovuti rasmi]

Maisha ya awali

Salmon alizaliwa mjini Bethnal Green, London, England, akiwa mtoto wa Sylvia Ivy Brudenell Salmon, nesi.[1] Makuzi yake yalikuwa mjini Luton na kuhitimu elimu ya msingi katika shule ya Ramridge Primary School halafu elimu ya juu Ashcroft High School.

Baada ya kumaliza shule, Salmon anakuwa mpiga dramu wa bendi ya rock maarufu Friction ambayo inaundwa na marafiki zake watoto waliokuwa wanasoma wote katika shule ya Ashcroft High School.[2] Bendi ilifanikiwa kutoa EP ya inchi 7, kaseti mubashara, kaseti-EP na kutumbuiza kawaida hasa katika mji wa Luton kati ya 1979 na 1980.[2] Salmon vilevile alifanya kazi na bendi nyengine maarufu kama Tee Vees.[2]

Marejeo

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: