Cagliari Calcio

Cagliari Calcio (maarufu kama Cagliari; matamshi ya Kiitalia: [ˈkaʎʎari]) ni klabu ya mpira wa miguu huko Italia. Klabu hii kwa sasa inacheza katika Serie A.

Uchezaji bora wa klabu hiyo Ulaya ulionekana kwenye mashindano ya kuwania Kombe la UEFA la mwaka 1993-94, ilitolewa na klabu ya Inter milan katika hatua ya nusu fainali.

Historia

Kabla ya Serie A

Klabu ya Cagliari (mwaka 1930-1931)

Cagliari walikuwa mabingwa wa kwanza wa Serie C wakati wa msimu wa mwaka 1951-52; kabla ya hapo kwenye ligi, ubingwa ulishirikisha timu zaidi ya moja.

Mnamo miaka ya 1950 Cagliari ilipandishwa Serie B.

Mnamo mwaka 1954 walishushwa na kupelekwa Serie C kwa sababu ya kushuka kiwango cha uchezaji. Baada ya kushuka kwenye Serie C mwanzoni mwa mwaka 1960, Cagliari iliongeza kasi na ubora wa uchezaji na hatimaye ikafanikiwa kupandishwa kwenye Serie A mnamo mwaka 1964.

Uwanja

Klabu ya Cagliari ilicheza katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mwaka 1970-2017

Klabu ya Cagliari ilihama kutoka katika uwanja wa Stadio Amsicora kwenda katika uwanja wa Stadio Sant'Elia mnamo mwaka 1970, baada ya kushinda taji lao pekee la ligi.

Mizozano na baraza la mji juu ya ukarabati wa uwanja ilimaanisha kuwa Cagliari alicheza michezo yao ya mwisho ya nyumbani ya mwaka 2011-12 huko Stadio Nereo Rocco katika Peninsula ya Italia.

Kwa misimu mingi uliofuata, klabu ya Cagliari ilicheza kwenye uwanja wa Stadio Is Arenas karibu na manispaa ya Quartu Sant'Elena.Uwanja wa Sant'Elia ulibomolewa mnamo mwaka 2017, na kilabu ilihamia uwanja wa Sardegna Arena.

Heshima

Mataji ya kitaifa

  • Serie A:
    • Washindi (1): 1969–1970
  • Serie B:
    • Washindi (1): 2015–2016
  • Serie C / Serie C1:
    • Washindi (4): 1930–1931, 1951–1952, 1961–1962, 1988–1989
  • Coppa Italia Serie C:
    • Washindi (1): 1988–1989
  • Campionato Sardo di I Divisione:
    • Washindi (1): 1936–37

Mataji ya Ulaya

UEFA Cup:

  • Hatua ya nusu fainali (1): 1993–1994

Wachezaji

Kikosi cha sasa( mwaka 2020)

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na.NafasiMchezaji
1 GKRafael
3 DFFederico Mattiello (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Atalanta B.C.)
4 MFRadja Nainggolan (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Inter Milan)
8 MFLuca Cigarini
10 MFJoão Pedro
12 DFFabrizio Cacciatore
15 DFRagnar Klavan
17 MFChristian Oliva
18 MFNahitan Nández
19 DFFabio Pisacane
20 MFGastón Pereiro
Na.NafasiMchezaji
21 MFArtur Ioniță
23 DFLuca Ceppitelli (Kapteni)
24 MFPaolo Faragò
26 FWDaniele Ragatzu
28 GKAlessio Cragno
30 FWLeonardo Pavoletti
33 DFLuca Pellegrini (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Juventus)
34 GKGiuseppe Ciocci
40 DFSebastian Walukiewicz
43 FWAlberto Paloschi (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya SPAL)
90 GKRobin Olsen (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya A.S. Roma)
99 FWGiovanni Simeone (amenunuliwa kwa mkopo kutoka klabu ya Fiorentina)

Barani Ulaya

Kombe la mabingwa wa Ulaya

MsimuMzungukoKlabuNyumbaniUgeniniJumla
1970–1971Mzunguko wa kwanza Saint-Étienne3–00–13–1
Mzunguko wa pili Atlético Madrid2–10–32–4

Kombe la UEFA

MsimuMzungukoKlabuNyumbaniUgeniniJumla
1972–1973Mzunguko wa kwanza Olympiacos0–11–21–3
1993–1994Mzunguko wa kwanza Dinamo București2–02–34–3
Mzunguko wa pili Trabzonspor0–01–11–1
Mzunguko wa tatu Mechelen2–03–15–1
Robo fainali Juventus1–02–13–1
Nusu fainali Inter Milan3–20–33–5


Tazama pia

Viungu vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: