Alfa na Omega

Alfa (Α au α) na omega (Ω or ω) ndizo herufi ya kwanza na ya mwisho ya alfabeti ya Kigiriki.

Herufi kubwa alfa na omega.

Kwa sababu hiyo zimechukuliwa kama ishara ya mwanzo na mwisho.

Kitabu cha Ufunuo (1:8, 21:6 na 22:13)[1] kinazitumia pamoja kama jina la Yesu Kristo na la Mungu[2][3], kwa kuwa ndio asili na kikomo cha viumbe vyote.

Picha

Katika Uyahudi

Maandishi ya Uyahudi yanasema kuwa neno emet (אמת, yaani "uaminifu"), moja ya sifa kuu za YHWH, linaundwa na herufi ya kwanza, ya kati na ya mwisho wa alfabeti ya Kiebrania.

Katika Uislamu

Qur'an (57:3) inataja al'Awwal (الأول), yaani "Wa Kwanza" na al'Akhir (الآخر), yaani "Wa Mwisho" kati ya majina ya Allah.

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alfa na Omega kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.