Aftermath Entertainment

Aftermath Entertainment ni studio ya kurekodi iliyoanzishwa na msanii na mtayarishaji wa muziki wa hip hop Dr. Dre. Inafanya kazi kama kampuni tanzu na vilevile kusambaziwa kazi zake kupitia kampuni ya Interscope Records ambayo ni mali ya Universal Music Group.

Aftermath Entertainment
Shina la studioUniversal Music Group
Imeanzishwa1996
MwanzilishiDr. Dre
Usambazaji wa studioInterscope Geffen A&M
(Nchini Marekani)
Polydor Records
(Nchini Uingereza)
Universal Music Group
(Dunia Nzima)
Aina za muzikiHip hop
NchiMarekani
MahalaSanta Monica, California
Tovutiaftermathmusic.com

Washirika waliopo sasa ni pamoja na Dr. Dre mwenyewe, Eminem, Kendrick Lamar na Jon Connor ikiwa na wasanii wa zamani akiwemo 50 Cent, Busta Rhymes, Game, Eve, Raekwon, Rakim, Slim the Mobster, Stat Quo na wengine wengi tu. Studio imefanya kazi miaka kadhaa na kujipatia tunukio kadha wa kadha za platinum 16 au zaidi katika matoleo yake yote ya albamu 20.

Historia

Alipoondoka Death Row Records mnamo Machi 22, 1996, Dr. Dre alianzisha Aftermath Entertainment kupitia Interscope Records.[1] Albamu ya Dr. Dre Presents: The Aftermath ilitolewa mwishoni mwa mwaka wa 1996 ikishirikisha wasanii ambao walikuwa miongoni mwa washirika wa mwanzo wa lebo hiyo. Mnamo mwaka wa 1997, Aftermath ilitoa albamu pekee ya kushirikiana ya kundi la muziki wa hip hop la The Firm (liliundwa na Nas, Foxy Brown, AZ na Nature). Licha ya albamu kuhusisha utayarishaji kutoka kwa Dr. Dre mwenyewe na kushika nafasi ya juu kwenye chati ya Billboard 200 na kuthibitishwa kuwa platinamu, ilikuwa na mauzo chini ya matarajio ya kibiashara na baadae kundi lilisambaratika.

Baada ya mapendekezo kutoka kwa mkurugenzi wa Interscope Jimmy Iovine, Dr. Dre alimsaini Eminem mnamo Machi 9, 1998.[2] Mwaka uliofuata (1999), albamu ya kwanza ya Eminem, The Slim Shady LP ilitolewa. Albamu ilishika nafasi ya pili kwenye Billboard 200 na nambari moja kwenye chati ya "Top R&B/Hip-Hop Albums". Albamu hii imethibitishwa kuwa platinamu mara nne, na bila shaka ndio albamu ya kwanza yenye mafanikio katika lebo hiyo. Mwaka 1999, Aftermath ilitoa 2001, ni albamu ya pili ya Dr. Dre baada ya "The Chronic". Albamu hii imethibishwa kifikisha mauzo ya platinamu mara sita.

Wasanii wengine kadhaa walisainiwa na baadaye wakaondoka kwenye lebo ya Aftermath, baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Hittman na Rakim kutokana na migogoro ya utayarishaji. Matatizo ya kisheria yalimlazimu mwimbaji Truth Hurts kuondolewa katika lebo baada ya kutolewa kwa albamu yake.[3]

Mnamo 2002, rapa kutoka jiji la New York 50 Cent alisainiwa na Aftermath na Dr. Dre baada ya kusainiwa na Interscope kupitia Shady Records ya Eminem.[4] Albamu ya kwanza ya 50 Cent ya Get Rich or Die Tryin' ilitolewa mnamo Februari 6, 2003 kupitia Aftermath. Albamu ya Get Rich Or Die Tryin' ilihusisha utayarishaji wa Dr. Dre, ambaye pia alikuwa mtayarishaji mkuu wa albamu hiyo. Kutokana na mafanikio ya wimbo wa 21 Questions, albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Billboard Top 200. Kwa kuuza nakala 872,000 katika wiki yake ya kwanza, albamu hiyo iliidhinishwa kufikisha mauzo ya platinamu mara 9 nchini Marekani mwaka wa 2020.

Game, ambaye alisainiwa na lebo hiyo mwaka 2003, alitoa albamu yake ya kwanza ya The Documentary kwa ubia na G-Unit Records mwaka 2005. Muda mfupi baada ya kutoka kwa albamu ya "The Documentary", ulizuka mvutano kati ya The Game na 50 Cent na kusababisha The Game kuondoka kwenye lebo mwaka wa 2006.

Busta Rhymes pia alitiwa saini na lebo hii na kuachia albamu moja kabla ya baadaye kuondoka kwenye lebo kutokana na mzozo na mkurungezi wa Interscope, Iovine. Albamu yake ya Back on My B.S. ilipangwa kutolewa na Aftermath. Baadae aliposaini mkataba na Universal Motown iliripotiwa kwamba albamu hiyo itatolewa kwenye lebo yake, Flipmode Entertainment, kupitia mkataba wake na Universal Motown.[5] Stat Quo pia aliondoka kwenye lebo hii mwaka wa 2008, chanzo kikitajwa kuwa ni tofauti za mwelekeo wa kisanaa.[6]

Mnamo Januari 2010, ilitangazwa kwamba Bishop Lamont ameachana na lebo hiyo kutokana na kuchelewa mara kwa mara kwa albamu yake ya kwanza, The Reformation,[7] wakati huo huo mwimbaji wa muda mrefu wa Aftermath, Marsha Ambrosius, pia alikuwa ameachana na lebo hiyo.[8]

Mnamo Machi 8, 2012, ilitangazwa kuwa Kendrick Lamar alikuwa amesaini rasmi na lebo hiyo.[9]

Mnamo Oktoba 15, 2013, Jon Connor alitangaza kusaini kwake na Aftermath wakati wa Tuzo za BET Hip Hop za 2013.[10]

Mnamo Februari 20, 2014, 50 Cent alitangaza kuachana na mkataba wake na Interscope ambao ulijumuisha mkataba wake na Aftermath na Shady.[11]

Tarehe 7 Agosti 2015, Dr. Dre alitoa albamu yake, Compton. [12]

Wasanii

Wasanii wa sasa

MsaniiMwaka
aliosainiwa
Matoleo

chini ya lebo

Dr. DreMwanzilishi2
Eminem199811
Kendrick Lamar20125
Anderson .Paak[13]20162
Silk Sonic20211

Wasanii wa zamani

MsaniiMiaka ndani
ya lebo
Matoleo
chini ya lebo
Group Therapy1996—1997
The Firm1996—19981
RBX1996—1999
King T1996—2001
Dawn Robinson1997—2001
Hittman1998—2000
Rakim[14]2000—2002
The Last Emperor2000—2003
Truth Hurts2001—20031
50 Cent[15]2002—20145
The Game2003—20061
Stat Quo2003—2008
Eve1998
2004—2007
Busta Rhymes2004—20081
Dion[16]2005—2007
G.A.G.E.[17]2005—2007
Raekwon2005—2008
Bishop Lamont2005—2010
Joell Ortiz2006—2008
Marsha Ambrosius2006—2009
Hayes[18]2009—2010
Slim the Mobster2009—2012
Jon Connor2013—2019
Justus2015—2016

Watayarishaji muziki wa sasa

  • Dawaun Parker
  • Dem Jointz
  • DJ Khalil
  • Erik "Blu2th" Griggs
  • Focus...
  • Fredwreck
  • Mark Batson

Watayarishaji muziki wa zamani

Tanbihi

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aftermath Entertainment kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.