Uenezi wa lugha za Wabilikimo katika Afrika ya leo kadiri ya Bahuchet (2006). Watwa wa Kusini hawaonyeshwi.Wabilikimo wa kabila la Wabaka wa Kamerun wakicheza.
Wabilikimo (yaani watu bila kimo) ni binadamu wa makabila ambayo miili yao ni mifupi kuliko kawaida. Wataalamu wanatumia jina la Kiingereza lenye asili ya Kigiriki[1]Pigmy kwa wasiofikia sm 150[2]na pygmoid kwa waliozidi kidogo kipimo hicho.[3]
Makabila ni tofauti kati yake, lakini ni tofauti zaidi sana na binadamu wengine. Vipimo vya DNA vinadokeza kwamba wana asili moja, ya zamani sana (miaka 60,000 hivi iliyopita[7]) kuliko aina nyingine zote za watu isipokuwa Wasani.[8]
Mbali na makabila ya Wabilikimo, kuna watu katika makundi yoyote ya jamii ambao wanaweza kuwa wafupi kupita kiasi kwa sababu 300 na zaidi tofauti za kiafya. Mtu wa namna hiyo kwa Kiingereza anaitwa dwarf.